Kusuhu Sisi Umoja ni Nguvu - Mbezi Luis

Wazo la kuwa na umoja lilianza katika Jumuiya ya Mt. Gabriel wa  Meteso mwaka 2004. walioshiriki mchakato huo ni Flavian Mgomela, Ananias Ngugo, Adam Kiheka, Avitus Rwezaula,Respicius Rutta,Sylivester Matiku, Dr. Santois Lyando,Adelina Katwanga,Gerald Lwila,Lemi,Yohana Napake bila kuwasahau Baltazar Magashi, Emmanuel Masanja, Peter Maliwa maarufu “Jina langu linavuma….”na Daniel Malimi “Sabodo

Mwaka 2007 rasmi Umoja ni Nguvu ilianzishwa baada ya kujitenga kutoka kwenye Jumuiya na kuwa umoja wa kijamii. Viongozi  kwanza walikuwa:

  1. Mwenyekiti – Flavian Mgomela
  2. Katibu –  Ananias Ngugo
  3. Mtunza hazina   –  Jane Santos

Mwaka 2010 tulipitisha dua ya umoja pamoja na kanuni ya kukokotoa kiingilio cha mwanakikundi mpya kwa uratibu wa mzee wetu Yohana Napake.

Ujumbe wa Mwenyekiti Umoja ni Nguvu

Maisha yetu binadamu yamejaa “Sinto-fahamu” nyingi. Hivyo, Mtaji wetu mkubwa sisi Umoja Ni Nguvu ni Watu wetu, upendo wetu, uwajibikaji wetu na utayari wetu wa haraka wa kujitoa kwetu kwa ajili ya kumusaidia mwenzetu kukabiliana na sinto-fahamu iliyomupata.

Umoja ni Nguvu Mbezi Luis Tunahitaji na tumeweza !

Alexius Kasigara Kanyambo
Mwenyekiti, Umoja Ni Nguvu- Mbezi Luis
2014-2016 na 2021-2025

Viongozi Wetu Kutana na Viongozi wa Umoja ni Nguvu

Matukio mbalimbali Matukio mbalimbali yaliyotekea kwenye umoja wetu